Featured
Loading...

BWAWA LA KUPONYA WATU NIGERIA LAWA GUMZO BAADA YA WATU HAO KUVUA NGUO HADHARANI

Watu mbalimbali wenye magonjwa wakimiminika kwenye maji ya bwawa nchini Nigeria na kuoga wakiwa na imani ya kuponywa magonjwa yao. Watu hao wakiwemo wazee, vijana waume kwa wake na wenye magonjwa mbalimbali wamekuwa wakizama kwenye maji hayo kwa urefu wa futi tatu hadi nne, wengi wakiwa uchi au nguo za ndani tu.

Wengine huchota maji hayo na kuosha sehemu yenye tatizo hasa wale wenye kushindwa kuona au wenye vidonda sugu kama vile kansa, Ukimwi nakadhalika.

Bwawa hilo limepewa jina la Orimiri lipo umbali wa kilomita 3 kutoka mji wa Nachi, Enugu nchini humo na liligunduliwa na watu wa Kabila la Fulani.

Post a Comment

CodeNirvana
Newer Posts Older Posts
© Copyright entertainment | Designed By Code Nirvana
Back To Top