MSAMAHA: Mwanahamisi ambaye ni mke wa mtu akiomba samahani baada ya kunaswa.
Tukio hilo la kufedhehesha lilijiri hivi karibuni, mchana kweupe nyumbani kwa wanandoa hao maeneo hayo.
ILIKUWAJE?
Kwa mujibu wa mtu wa karibu wa wanandoa hao, mume wa Mwanahamisi aitwaye Mashaka au baba Daudi ana rafiki yake aliyetajwa kwa jina moja la Paulo ambaye alidai kusumbuliwa na shemeji yake (mama Daudi) kwa muda mrefu.
Ilidaiwa kuwa mama Daudi alikuwa akimtumia Paulo ujumbe wa mapenzi kupitia simu hadi wakati mwingine kufikia hatua ya kumbana na kumkumbatia pale anapokutana naye njiani.
Ikaelezwa kwamba Paulo alimwambia baba Daudi kuwa alikuwa ameshamtumia zaidi ya SMS 240 za kimapenzi.
Baada ya kuona kero zimezidi huku rafiki yake akimlalamikia kutomuelewa mke wake aliyezaa naye mtoto mmoja ambaye bado hata hajaacha kunyonya, Paulo aliamua kuvunja ukimya na kumuonesha ujumbe anaotumiwa na shemeji yake huyo ili wamkomeshe.
AIBU YA USALITI: Mke wa mtu pamoja na njemba aliyokuwa nayo wakiwa na aibu baada ya kunaswa live chumbani.
Ilisemekana kwamba baada ya kufanya tathmini ya SMS hizo, baba Daudi na Paulo waliweka mtego huku wakimshirikisha mke wa Paulo ambaye aliwahi kugombana na mama Daudi kwa kitendo cha kumtambia ovyo.
Ilielezwa kuwa baada ya mpango kukamilika huku Paulo akimwambia shemeji yake kuwa amemkubalia, mama Daudi alimuaga mumewe kuwa baba yake ni mgonjwa huko Yombo-Buza, Dar hivyo anakwenda kumuona na siku hiyo atarudi saa 12:00 jioni akijua kuwa kwa mwanya huo ataweza kwenda gesti maeneo ya Ukonga-Mombasa, Dar na Paulo kama walivyokubaliana.
Ilisemekana kuwa baada ya Paulo kuona gesti patakuwa na shida ya kumshikisha adabu mama Daudi, alimshawishi wakutane chumbani kwa mumewe (baba Daudi) ili iwe rahisi kumfumania.
Ilifahamika kwamba ili kusaliti chumbani kwa mumewe, alimpigia simu baba Daudi kujua alipokwenda.
Kwa kuwa baba Daudi alijua mchezo, alimwambia mkewe kuwa amekwenda kufuatilia kitambulisho cha kazi kisha atakwenda Kigogo, Dar kwenye mishemishe nyingine.
Ilidaiwa kuwa majibu hayo yalimfurahisha mama Daudi ambaye alimwalika Paulo chumbani kwa mumewe bila kujua aliwekewa mtego.
Post a Comment