Umaarufu wake uliongezeka zaidi pale alipokamatwa na madawa huko Afrika Kusini, jambo lilomfanya anyee debe kidogo kabla ya kuachiwa na kurudi uraiani kwa mbwembwe zote. Ikapita miezi michache akarudi bongo huku akiwa mtu huru kabisa.
Wiki chache zilizopita Agnes aliamua kurudi sauzi kwa yule mchumba wake aliyekoswa koswa kukamatwa nae na madawa ya kulevya na tetesi zinasema kua alirudi sauzi kumpa taarifa bwana wake huyo kua yeye kwa sasa ni mjamzito.
Tetesi hizo zimethibitishwa jana pale Agness alipoamua kuweka picha yake Instagram na kuandika " Mama Kijacho " Ikimaanisha kua siku si nyingi ataingiza kiumbe kipya duniani. Inadaiwa kua Mchumba wake huyo kwa furaha aliyoipata baada ya kupewa taarifa hizo aliamua kumvalisha pete ya uchumba kabisa.
Habari BongoClan tulizozipata kutoka kwa ndugu wa karibu wa Agness ambae hakutaka kutajwa jina lake ni kua Mchumba wake huyo anaplan za kuja Bongo kutoa mahari kabisa ili baada ya Masogange kujifungua wafunge Pingu za maisha.
Post a Comment