1.jiandae kisaikolojia kuhusiana na usahili wenyewe hadi wiki moja ama mbili kabla,tenga muda wa kupitia mambo muhim yanayohusika na usahili huo.mfano kama ni usahili wa uhamiaji jiulize wahamiaji jiulize maswali "wezekana"(possible questions),mfano ni maeneo gan ambayo ni point kuu ya wahamiaji,waweza pia kukaa na mtu ambaye tayar alishafanya usahil huo ama mfanyakazi ya idara hiyo akakupa dondoo zaidi
2.Fika kituo cha usahili mapema kama masaa mawilu ama saa moja kabla ili kujijenga kisaikolojia na kuendqna na mazingira,sio dakika kumi ama tano kabla ya usahili.jadiliana na wenzako mnaofanya nao usahili na jiamini kwamba utafaulu.
3.vaa mavazi nadhifu na ya kiheshima,mfono usiende katika usahili wa sekta ya serikal ama popote ukiwa umevaa jinz tena mlegezo,ama kwa akina dada msivae nguo fupi.pia kuvaa micheni mibangili na urembo usiokuwa na tija kwa wakat huo muhimu kwako.
Kwa wanaume vaa surual nzur ya kitambaa ama kadet na shati chomekea(sio lazima),nyoosha nguo vizur na kiatu kiwe katika hali nzuri.
4.ukiwa katika chumba cha usahili,usiogope wala kujibu kwa panic!,jibu kiutulivu maswali yote na kama hujaelewa swali uliza sio kwenda nje ya point.usiongee kwa mbwembwe na nyodo ama kwa kuonesha vidole(body languages)maana kuna baadhi ya wasahili hawapendi.kutulia kwako katika kujibu maswal kutakuongezea nafasi wa kufaulu.kama interview n ya kiingereza usiongee kiingereza cha mtaani wala kutoka puani maana inatuchukiza wasahili wengi.simama kwa unyenyekevu na ikibidi anza kwa kusalimia kama inawezekana.msikilize muulizaji vizur na mwangalie usoni sio chini,wakat wa kujibu pia angalia wasahili usoni
5.ukisahihishwa jambo ama kukosolewa, kubali na usiwe na jazba hata kama unajua uko sahihi maana mara nyingine huwa tunafanya hivo ili kuona kama we ni mvumilivu kiasi gan ama kama unahasira za haraka ama unakata tamaa mapema
6.baada ya kumaliza usahili aga kama inawezekana na toka nje kwa adabu na utii kama ulivoingia.
Post a Comment