Mmiliki wa club ya soka ya Manchester United Malcolm Glazer alieinunua club hiyo toka mwaka 2005, amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 85 huku akiacha mke, watoto sita na wajukuu kumi na nne. Glazer aliyekua akiishi Palm Beach Florida Marekani, amekua akiugua kwa miaka kadhaa hivi sasa na biashara zake kama club ya Manchester United zimekua zikiendeshwa na familia yake.

Siku ya leo May 28 2014 ni mwaka mmoja umetimia toka afariki staa wa bongofleva Albert Mangweha ambapo leo hii dunia imepata misiba miwili mikubwa ambapo mmoja ni wa
Mwanaharakati, mshairi na mwandishi mahiri wa vitabu duniani Maya Angelou pamoja na Malcom Glazer.
Wednesday, 28 May 2014
Post a Comment