Mama huyo akiwa hoi baada ya kipigo toka kwa wanachi wenye hasira.
THIS IS NOT FAIR: Wimbi la wananchi kujichukulia sheria mkononi limezidi kushika kasi nchini Tanzania. Ikiwa hazijapia siku nyingi toka mwanafunzi wa chuo kikuu Ruaha kuuawa kwa kuchomwa moto kwa madai ya wizi. Taarifa tulizozipata leo asubuhi toka Kilema, Moshi Vijijini mkoani Kilimanjaro, mama mmoja inayesemekana ni kichaa amepigwa na wananchi wanaojiita wenye hasira kwa kumuhisi ni mchawi baada ya kukutwa akiwa mtupu hajitambui kwenye mfereji...
Baada ya kumuuliza na yeye kushindwa kuongea chochote ndipo walipoanza kumshushua kichapo kwani hakuna aliyekua akimfahamu maeneo hayo maskini!
Kwa bahati nzuri akaja kuokolewa na askari na kupelekwa hospitali, baada ya kupimwa ndipo ilipogundulika kuwa kumbe ni kichaa!
Post a Comment